Wezi wa Divai ya kanisa na kula Sakramenti wasakwa na police Kenya

Polisi Nchini Kenya wameanzisha uchunguzi kufuatia uvamizi katika kanisa la Kirinyaga ambapo wezi  walivamia na kunywa  divai ya madhabahuni huku wakishiriki kula mkate wa sakramenti pia kuondoka na mali ya kanisa.

Tukio hilo lilitokea katika kanisa la ACK St. Matthew’s Mutithi ambalo  liliwaacha Wakaazi wa eneo hilo na mshangao mkubwa kutokana na kisa hicho kilichotokea .

Kwa mjibu wa taarifa ya Naibu mwenyekiti wa kanisa hilo Eliud Githaka amesema wizi huo uliripotiwa na wanakwaya ambao waligundua kinanda hakipo huku Mlinzi wa usiku akituhumiwa kulala kazini kwani wizi huo ulitokea akiwa kazini.

Wakaazi wa eneo hilo wanadai kuwa Mlinzi huyo hakutambua kuwa kanisa lilikuwa limevunjwa ambapo Maafisa wa polisi walitembelea kanisa hilo Jumatatu usiku na kuwahakikishia waumini kwamba uchunguzi unaendelea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii