MBUNGE KENYA ATUPWA KATIKATI YA SHAMBA

Nchini  Kenya Mbunge wa Juja George Koimburi amekutwa ametupwa akiwa hai katikati ya shamba la kahawa katika kaunti ya Kiambu nchini humo baada ya kukamatwa na watu wasiojulikana nje ya kanisa katika eneo la Mugutha mei 25,2025.

Kwa mujibu wa video fupi za CCTV zilionesha mbunge huyo alichukuliwa kwa nguvu na watu wasiojulikana na kuondoka naye huku wakitumia gari aina ya Subaru Forester yenye rangi ya silver na kumwacha mkewe akiwa na majeraha makari kutokana na purukushani hizo.

Aidha idala ya Upepelezi na Makosa ya Jinai nchini Kenya imekana kuhusika na tukio hilo licha ya kuthibitishwa kwamba mbunge huyo amekuwa akitafutwa tangu Ijumaa kutokana na matukio ya udanganyifu wa ardhi na matumizi mabaya ya fedha za mfuko wa jimbo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii