Diwani wa Kiwere Felix Waya amefariki dunia ghafla jana Mei 23, 2025 baada ya kumaliza kuhutubia katika mkutano wa ziara ya CCM uliofanyika katika ukumbi wa Masai uliopo kwenye kata hiyo Wilaya ya Iringa.
Akizungumza na Mwananchi leo Mei 24, 2025 Katibu wa UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini Mfaume Gomangulu amesema kifo cha Diwani Waya ni cha ghafla na kimetikisa chama na jamii kwa ujumla.
Emeeleza kuwa baada ya Waya kumaliza kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wananchi katika mkutano wa hadhara, alisema anahisi hayupo sawa na akaomba kutoka nje apunge upepo lakini muda mfupi baadaye alisema anajisikia vibaya akapelekwa haraka katika Kituo cha afya Nzihi, lakini hali yake ilionekana kuwa mbaya zaidi na hivyo akakimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa.
Dwani huyo alikuwa ni kiongozi mwenye historia ya kujitolea na utumishi kwa wananchi ambapo alianza uongozi wake kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambako alihudumu kuanzia mwaka 2015 hadi 2020.
Baadaye alijiunga na CCM na kuchaguliwa tena kuongoza Kata ya Kiwere kwa kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025, mauti yalipomfika.
Bwana alitoa na sasa ametwaa jina lake lihimidiwe ami