CHUO KIKUU CHA HARVARD KUTOPOKEA WANACHUO WA KIGENI

Serikali ya Marekani imekizuia Chuo Kikuu cha Harvard kuandikisha Wanafunzi wa Kigeni ambapo imaelezwa imechukua hatua hiyo kwa kuwa #Harvard inaiunga Mkono Palestina pamoja na kushirikiana na Chama cha Kikomunisti cha China

Barua imetolewa na DonaldTrump iliyokuwa ikielekezwa kwa Uongozi wa Chuo hicho kuwa Cheti cha Usajili cha Mpango wa Kubadilishana Wageni (Student Exchange Visitor Program – SEVP) cha Chuo hicho kimefutwa rasmi.

Chuo cha Harvard kina jumla ya Watu 9,970 katika kundi lake la Taaluma ya Kimataifa na takwimu zinaonesha Wanafunzi wa Kimataifa 6,793 wanachangia 27.2% ya Usajili wake kwa Mwaka wa Masomo wa 2024–2025.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii