Polisi mjini Naivasha wamemkamata mwanamume mmoja raia wa Uganda kwa madai ya kumuua mkewe katika eneo la Lwakhakha linalopakana na Kenya na Uganda.
mshukiwa alimdunga kisu mkewe wa miaka 28 hadi akafariki kwa sababu ya kupika omena badala ya nyama kwa chakula cha jioni. Ripoti ya polisi ilionyesha kuwa mshukiwa alimshambulia mkewe Ijumaa, Machi 14, katika kijiji cha Bukitongo B, kata ndogo ya Bumwoni, wilaya ya Namisindwa, kabla ya kutorokea eneo lisilojulikana.
Mtoto wao wa miaka 10 aliwaambia majirani kuwa ugomvi ulianza baada ya babake kurejea nyumbani na kukuta omena na ugali badala ya nyama.