Ndege zisizo na rubani za Sudani zashambulia mji wa mpakani karibu na Eritrea

Wanajeshi wa Sudani wamefanya shambulio la nadra la ndege zisizo na rubani katika mji wa mashariki wa Kassala, karibu na mpaka wa Eritrea, chanzo katika serikali pinzani, inayoshirikiana na jeshi, kimesema Jumamosi.

"Ndege isiyo na rubani ililenga eneo la kuhifadhi mafuta katika uwanja wa ndege wa Kassala," chanzo cha serikali kimeliambia shirika la habari la AFP, kikilaumu shambulio hilo la Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF), bila kuripoti majeruhi au uharibifu wowote.

Tangu mwezi Aprili 2013, jeshi la serikali, likiongozwa na Jenerali Abdel Fattah Abdelrahman Burhan, kiongozi wa Sudani limekuwa likipigana na RSF, inayoongozwa na Mohamed Hamdane Daglo, katika vita vya kikatili vilivyosababisha makumi kwa maelfu ya raia kuuawa na mamilioni ya wengine kuyahama makazi yao.

Wakati mzozo huo unapoingia mwaka wake wa tatu, nchi hiyo ya tatu kwa ukubwa barani Afrika imegawanyika: jeshi linadhibiti katikati, mashariki na kaskazini, wakati RSF inatawala sehemu kubwa ya eneo la magharibi la Darfur na sehemu za kusini.

Kassala iko kama kilomita 400 kutoka ngome ya karibu inayojulikana kushikiliwa na RSF, kusini mwa Omdurman, mji pacha wa mji mkuu.

Pia ni takribani umbali sawa na maeneo yanayodhibitiwa na washirika wa RSF, tawi la Sudan People's Liberation Movement-North (SPLM-N) linaloongozwa na Abdelaziz al-Hilu.

Mwishoni mwa mwezi wa Februari, wanamgambo na washirika wao walitia saini mkataba nchini Kenya kutangaza mpango wa kuanzisha serikali pinzani kwa ile yenye makao yake makuu katika mji wa Port-Sudani.

Pia siku ya Jumamosi, chanzo cha kijeshi kimeliambia shirika la habari la AFP kwamba ndege ya mizigo ililengwa katika uwanja wa ndege wa Nyala, mji mkuu wa jimbo la Darfur Kusini.

Chanzo hicho kilisema kuwa ndege hiyo ilitua kwa minajili ya kusambaza chakula na risasi kwa wapiganaji wa RSF, bila kutaja ni nani aliyeilenga.

Mashahidi waliripoti kusikia mlipuko mkubwa mapema asubuhi ukitokea eneo la uwanja wa ndege.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii