Jeshi la Sudan Kusini linasema linaudhibiti tena Mji wa Nasir

Msemaji wa jeshi la Sudan Kusini, amesema kuwa vikosi vya serikali vimeuteka tena mji wa Nasir ambao umekuwa kitovu cha mzozo wa kisiasa ambo umekuwa ukitokota nchini humo.

Machafuko katika mji wa Nasir katika jimbo la Kaksazini mashariki la Upper Nile, yametishia kuitumbukiza tena Sudan Kusini katika mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Washirika wa Kiir wanashutumu vikosi vya Machar kwa kuchochea machafuko huko Nasir kwa kushirikiana na kundi cla vijana wenye silaha la Whitearmy kutoka jamii ya kabila la Nuer la makamu wa rais wa Kwanza Riek Machar

Mapema mwezi Machi, takriban wapiganaji wa elfu 6 wa kund la White Army walivamia kambi ya kijeshi katika mji wa Nasir, kumuua jenerali mkuu na wengine wengi.

Jeshi la sudan kwa kusaidiwa na jeshi la Uganda, limekuwa likipambana kuudhibiti tena mji huo.

Juma hili pia, jeshi lilitangaza kuteka mji wa Ulang ambao kwa muda mrefu umekuwa ukidhibitiwa na vikosi vya Machar.

Mzozo wa hivi karibuni kati ya rais Salva Kiir na makamu wake Machar umetishia kuvunjika kwa makubaliano ya amani ya 2018.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii