Waziri Gwajima Akerwa na Udhalilishaji wa Mabinti Chuoni, Achukua Hatua

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima ameeleza kusikitishwa juu ya kitendo cha mabinti kadhaa wa chuo kikuu wakishirikiana kumdhalilisha binti mwingine kwa maneno na vipigo, huku sababu zikiwa ni kumgombania mwanaume aliyetajwa kwa jina moja la Mwijaku.

“Binafsi, nimesikitishwa sana kusikia mabinti wasomi ambao wangetakiwa kujikita kwenye elimu na kuunganisha nguvu kupambana kutokomeza ukatii dhidi ya wanawake na watoto, badala yake wanatumia nguvu zao na elimu zao kukatiliana, kudhalilishana na kujidhalilisha wao kwa wao. Udhalilishaji walioufanya kwa binti mwenzao haukubaliki kabisa na unastahili kukemewa kwa nguvu zote,” amesema

Kupitia taarifa yake, Dkt. Gwajima ameeleza hatua alizochukua kufuatia tukio hilo ikiwa ni pamoja na kuwasiliana na wakuu wa vyuo husika kupitia madawati ya jinsia kwenye vyuo husika ili hatua za kinidhamu zichukuliwe kupitia sheria na miongozo ya vyuo husika dhidi ya waliotekeleza udhalilishaji huo.

Ameongeza kuwa “Nawasiliana na Waziri mwenye dhamana na Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani kwa hatua zaidi.”

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii