Madereva Watanzania Wakwama Goma, Wazungukwa na Milio ya Risasi Kila Kona

Kutokana na machafuko yanayoendelea nchini Congo na jitihada za waasi wa kundi la M23 kupambana kuuchukua mji wa Goma, madereva wa magari makubwa ya mizigo(Malori) ambao ni watanzania wamekwama katika eneo la Jambo Safari katika mji wa Goma.

Kupitia video inayosambaa katika mitandao ya kijamii madereva hao wameeleza kuwa hali sio nzuri katika eneo walilopo na wana takribani siku nne wamekwama.

Mmoja wao amejitambulisha kama Aloyce Emmanuel ambaye ni dereva wa kampuni ya RMD amesema “tunaomba msaada sisi huku tilipo hali ni mbaya”

Wakati wakiendelea kuzungumza imesikika milio ya risasi jambo linaloashiria wapo katika eneo ambalo si mbali na mapigano yanapoendelea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii