XZIBIT ATOA SABABU ZA DRAKE KUSHINDWA NA KENDRICK LAMAR

Rapa kutoka Marekani Alvin Nathaniel Joiner maarufu kama Xzibit ama Exhibit A . X to the Z. Wow Alvin.... Amesema kwamba ni kweli Drake alishindwa kwenye vita yake na Kendrick Lamar 

Kupitia mahojiano ambayo ameyafanya na The Drink Champ Xzibit ameweka wazi sababu zilizo mfanya Drake kushindwa na Kendrick Lamar 

Kwa mujibu wa Xzibit anasema kwamba Drake alimdharau mpinzani wake ... Na kilichotokea ni matokeo ya kumvaa mtu ambae humjui, Xzibit anatolea mfano kisa cha Daudi na Goliath ambapo anasema mwanzo Drake alikua anaongea sana na Kendrick Lamar alikua kimya tu

Kitendo cha Drake kutumia AI( Akili bandia ) yenye sauti ya 2 Pac kwenye wimbo wa  Taylor Made Freestyle... Xzibit anadai kwamba kiliwakwaza hata mashabiki wa West Coast na ndio maana kwenye wimbo wa Kendrick Lamar Not Like Us kuna mistari anaeleza juu ya jambo hilo

You think the Bay gon' let you disrespect Pac//

I think that Oakland show gon' be your last stop//

Sio mara ya kwanza kwa Xzibit kuzungumza na kutoa maoni yake kwenye vita kati ya Drake & Kendrick Lamar.... Mwanzo alizungumza na TMZ na kudai kwamba kuna vitu anajifunza kutoka kwa Kendrick Lamar lakipi pia alimpongeza Drake kwa kipaji chake na mwisho akatoa onyo kwamba vita hiyo inapaswa kuwa kwenye Muziki pekee na sio nje ya hapo

Kauli hiyo ilikua ni baada ya kutoka kwa taarifa mwaka jana kwamba kulisikika milio ya risasi karibu na nyumbani kwa Drake

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii