Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Omary Seleman Mwanamtwa (61), mkazi wa Morogoro ambaye ni dereva wa teksi, anashikiliwa na polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za mauaji ya mteja wake, Ulumbi Stephano (61).
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo mwaka 2016.
Amesema siku ya tukio, marehemu (Ulumbi) alikodi teksi kwa ajili ya shughuli zake binafsi, lakini siku hiyo hakuonekana hadi baadaye gari lake lenye namba za usajili T.577 AQJ aina ya Toyota Corolla lilipokutwa kwenye kituo cha mafuta likiwa na damu.
RPC Mkama amesema mtuhumiwa huyo anaendelea kuhojiwa, huku mwili wa marehemu huyo hadi sasa bado haujapatikana.