Miili yawaliouawa katika shambulio kwenye mkutano wa M23 yazikwa

Familia mashariki mwa DRC, Jumanne ya wiki hii zilizika wahanga wa shambulio lililoua takriban watu 13 huko Bukavu, huku jamaa waliokuwa na huzuni wakiisihi serikali kuhakikisha amani na usalama.

Majeneza 12 yalionekana yakiwa yamepangwa katika hospitali ya mkoa huko Bukavu.

Misalaba midogo ya mbao yenye majina ya marehemu, pamoja na tarehe ya kuzaliwa  na mahali pa kuzaliwa na kifo iliwekwa mbele ya jeneza.

Watu hao waliuawa  katika milipuko miwili ilioyotokea katika mkutano wa waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda, ambao wameuteka mji huo.

Idadi ya waliofariki kutokana na milipuko ya Februari 27 sasa imeongezeka hadi 17, Dunia Masumbuko Bwenge, aliyeteuliwa na M23 kuwa makamu wa gavana wa jimbo la Kivu Kusini.

Idadi iliyoripotiwa hapo awali ilikuwa 13, na 11 walifariki wakati wakiwasili hospitilini na watu wengine wawili walifariki kutokana na majeraha.

Bado haijafahamika ni nani aliyehusika na milipuko hiyo iliyotikisa Bukavu siku 11 baada ya M23 kuuteka mji huo.

Wapiganaji wa M23 pia waliteka mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma, mwishoni mwa Januari, kama sehemu ya upanuzi wa eneo la kundi hilo tangu lilipoibuka tena mwaka 2021.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii