• Alhamisi , Machi 13 , 2025

Hamas yakabidhi miili ya mateka, Israeli ikiachiwa huru wafungwa

Hamas wamekabidhi miili ya mateka wanne wa Israeli mapema siku ya Alhamisi, baada ya wafungwa wa Kipalestina ambao wamekuwa wakizuiwa magereza ya Israeli kuachiwa na kupelekwa kwenye ukanda wa Gaza.

Ofisi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, imethibitisha kupokelewa kwa miili ya mateka hao, na mchakato wa kuwatambua umeanza.

Mjini Ramallah, wafungwa wa Kipalestina waliokuwa katika magereza ya Israeli wamewasili kwenye mabasi na kukaribishwa na wapendwa wao.

Wafungwa hao walikuwa waachiwe Jumamosi iliyopita, lakini Israeli ilisitisha zoezi hilo kwa kulalamikia namna Hamas walivyokuwa wanawaachia huru mateka walio hao au waliouwa.

Wakati hayo yakijiri, mazungumzo kuhusu awamu ya pili ya kutekeleza mkataba wa usitishwaji vita, yanatarajiwa kurejelewa na tayari mjumbe wa Marekani kwenye eneo la Mashariki ya Kati Steve Witkoff, amesema hatua inapigwa kati ya Israel na Hamas.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika jijini Doha au Cairo, kujadili ni lini awamu ya pili ya utekelezwaji wa awamu ya pili utaanza.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii