Wakaazi wa kijiji cha Malelei Kaunti ya Lamu sasa wanalazimika kulala kwa miti licha ya kuwa na nyumba zao.
Wakaazi wa kijiji hicho ambacho kinapatikana katika wadi ya Witu wanalazimika kulala kwa miti kwa hofu ya kushambuliwa na wanamgambo wa kundi la kigadi la Al-Shabab.
Kwa mujibu wa ripoti, wakaazi wana mchana tu kuwa makwao na kufanya kazi zao za nyumbani kama vile ukulima na punde tu giza linapoingia wanakimbia kujificha kwenye miti
Katika mashambulizi ya hivi maajuzi, wanamgambo wamekuwa wakishambulia maboma ya wakaazi na kuwaua kikatili wengi wa wahasiriwa wakiwa wanaume.
Visa hivyo vimeshuhudia zaidi ya watu 15 kuuawa na zaidi ya nyumba 15 kuteketezwa
Mnamo Januari 10, 2022, watu wawili waliuawa na nyumba kadhaa kuteketezwa kufuatia shambulizi liliotekelezwa katika kijiji cha Salama, Kaunti ya Lamu.
Wakaazi wa Juhudi, Salama na Widhu eneo la Majembeni, Kaunti ya Lamu walilazimika kukesha kwenye kibaridi kikali kufuatia majibizano makali ya risasi.
Wakaazi wa walitoroka kutoka mbaoma yao, wakiamua kujisitiri usiku huo katika shule zilizoko karibu, idadi nyingine katika soka la Kibaoni na wengine hata kukesha vichakani .
Shambulizi hili linajiri siku chache tu baada ya wavamizi kumimina risasi kadhaa na kusababisha wkaazi wa Mejembeni kutoroka eneo hilo.
Katika kisa sawia mnamo Januari 3, wavamizi waliokuwa wamejihami kwa silaha zikiwemo panga na bunduki, waliauwa watu sita na kuteketeza nyumba kadhaa kabla ya kutoroka eneo la Widhu Majembeni, kaunti ya Lamu.
Kwa mujibu wa Kamishna wa Kaunti ya Lamu Irungu Macharia, mmoja wa muathiriwa aliuawa kwa kupigwa risasi, mwingine akakatwa hadi kuaga dunia huku wengine wanne wakiteketezwa wakiwa katika nyumba zao.