Kijana Adaiwa Kumuua Baba Yake, Mjumbe na Kumjeruhi Mwenyekiti wa Kijiji

Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa jina la Zuberi Habibu, Mkazi wa Kijiji cha Mandudumizi B, Kata ya Zombo, Kilosa mkoani Morogoro, anashikiliwa na vyombo vya ulinzi na usalama kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili na kumjeruhi mmoja.

Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Wilaya ya Kilosa ambaye ndiyo Mkuu wa Wilaya, Shaka Hamdu Shaka amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Dc Shaka amesema chanzo cha mauaji hayo ni mgogoro wa ardhi na waliouawa kwenye tukio hilo ni Habibu Liomite ambaye ni baba mzazi wa mtuhumiwa, Hassan Khalid ambaye ni Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huku Hamisi Msabaha ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji akijeruhiwa.

Amesema tayari mtuhumiwa huyo ameshakamatwa akisubiri taratibu nyingine za kisheria.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii