Mkazi wa Kijiji cha Mwamagunguli mkoani Shinyanga, Makoye Mayala (45) amejinyonga hadi kufa baada ya kumjeruhi kwa kisu mtoto wake, Anna Makoye (06) mwanafunzi wa shule ya msingi Mwamagunguli.
Chanzo cha kumjeruhi mtoto kinadaiwa kuwa ni ugomvi wa kifamilia, ambapo baada ya mkewe kukimbia, ndipo Makoye aliporudi ndani na kumjeruhi mwanae shingoni na kupoteza fahamu, na ndipo alipoamua kujinyonga akidhani amemuua mwanaye.