Tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.8 kwenye vipimo vya Richeter laua watu kadhaa

Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea siku ya Jumanne katika eneo la Himalaya la Tibet, kusini-magharibi mwa China, limesababisha vifo vya watu wasiopungua 53 na kusababisha kuporomoka kwa "majengo mengi", tetemeko la ardhi likikosika hadi nchi jirani ya Nepal.

Tetemeko la ardhi la kipimo cha 6.8 limepiga kitongoji cha Dingri, kilicho karibu na mpaka wa China na Nepal, saa 9:05  asubuhi saa za China, kulingana na shirika la tetemeko la ardhi la China (CENC). Utafiti wa Jiolojia wa Marekani (USGS) umeripoti ukubwa wa 7.1 kwenye vipimo vya Richter

Video zinazorushwa na televisheni ya taifa ya China CCTV zinaonyesha nyumba za rangi nyeupe zikiwa kwenye mwinuko, zenye kuta zilizodondoka na paa zilizoporomoka, huku mawe yakiwa yametapakaa chini.

Picha nyingine kutoka kwenye kituo hicho zinaonyesha magari yaliyofukiwa chini ya matofali au hata wateja wakikimbia wakiondoka katika duka wakati ambapo tetemeko la ardhi likisababisha bidhaa zikidondoka chini.

Wazima moto wakiwa wamevalia sare za rangi ya chungwa walifika katika eneo la tukio, huku kukiwa na vifusi na karibu manusura na wazee wakiwa wamevikwa blanketi, kulingana na video za CCTV.

"Watu 53 wamefariki na wengine 62 wamejeruhiwa," shirika la habari la serikali la Xinhua limesema. Ripoti ya awali ya muda iliripoti vifo vya watu 32.

"Mitetemeko imesikika kwa nguvu sana ndani na karibu na jimbo la Dingri na majengo mengi yameporomoka karibu na kitovu tetemeko hilo," CCTV imesema.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii