Mkazi wa Kigamboni Vicent Masawe(36)maarufu kwa jina la ‘Bwana harusi’ amepandishwa Mahakamani kisutu akikabiliwa na mashtaka mawili.
Mshtakiwa huyo.amepandishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka yake na wakili wa Serikali Frank Rimoy.
Wakili Rimoy amemsomea mashtaja hayo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki aliyesikikiza kesi hiyo.
Katika shtaka la kwanza, Vicent anadaiwa wizi wa gari Toyota Ractis likiwa na thamani ya Sh 15miloni ambalo ni mali ya Silvester Massawe, aliyempa kwa ajili ya shughuli ya harusi, lakini hakulirejesha.
Shtaki hilo anadaiwa kulitenda Novemba 15, 2024 eneo la Dar es Salaam.
Pia mshtakiwa huyo anadaiwa kujipatia Sh 3 miloni kwa njia ya udanganyifu kutoka kwa Masawe kwa madai kuwa atamrudishia.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo,mshtakiwa alikana kutenda makosa hayo na dhamana ipo wazi iwapo atapata wadhamini wawili watakao saini bondi ya Sh 5milioni kila mmoja.
Pia mshtakiwa ametakiwa kuwasilisha mali isiyohamishika yenye thamani ya Sh 9milioni.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 7 2025 mwakani itakapotajwa tena.