AKATWA MKONO KISA KUCHELEWA KURUDI NYUMBANI

#HABARI Happyness Khalfan (30) mkazi wa Kata ya Mwendakulima wilayani Kahama mkoani Shinyanga, amekatwa na kitu cha ncha kali katika mkono wake wa kushoto na mumewe Charles Peter mkazi wa Mwendakulima Kahama.


Akizungumza akiwa amelazwa katika kituo cha Afya Mwendakulima Happyness amesema siku ya tukio alitoka lakini bahati mbaya akachelewa kurejea nyumbani ndipo alipomkuta mumewe amechukia na kufanya kitendo hicho.

Afisa kliniki mwandamizi wa kituo cha Afya Mwendakulima Leonard Mabula amekiri kumpokea mwanamke huyo akiwa amejuruhiwa huku akiwa anavuja damu nyingi.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Janeth Magomi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba chanzo bado kinachunguzwa.

Kwa mujibu wa Kamanda Magomi tukio hilo lilitokea Desemba 15 lakini likafichwa, ila wasamaria wema wakaliripoti na mpaka sasa wanaendelea kumtafuta mume wa Happyness ambaye ametoroka baada ya tukio hilo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii