Baada ya kukutana na mwanamke kwenye mtandao wa kijamii, Muhammed alimpenda sana na kuchukua hatua kubwa ya kuwatembelea wazazi wake na kulipa mahari.
Hata hivyo, nia yake ya kumuoa mwanamke huyo ilivurugika alipogundua kuwa mchumba wake alikuwa amemficha kama anaujauzito.
Mimba hiyo ilikuwa ya wanamume mwingine na binti alimtelekeza mwanaume ambaye ni muhusika wa mimba na kwenda kwa Muhammad.
Muhammad nae alihisi kusalitiwa na kushtushwa na tukio hilo. Huku hisia zikizidi kupanda, Muhammed alivamia makazi ya wazazi wa mwanamke huyo na kutaka kurejeshewa mahari aliyokuwa amelipa.
mwanamume huyo aliyevunjika moyo lilisababisha mijadala mikali, huku hasira zikipamba moto pande zote mbili.
Baada ya mabishano makubwa na mazungumzo, familia ilikubali kurejesha mahari ya Muhammed, na kumruhusu kuachana na mwanamke huyo.