Majaji walimtia hatiani kijana wa Indianapolis Raymond Ronald Lee Childs kwa kuua watu 6 wa Familia yake huku kukiwa na mzozo juu yake kuondoka nyumbani bila ruhusa.
Raymond Ronald Lee Childs anashtakiwa kwa makosa sita ya Mauaji, shtaka moja la kujaribu kuuana kubeba bastola bila Leseni Hukumu imewekwa tarehe 7 Januari 2025.
Shtaka hilo la kujaribu kuua linamhusu kaka yake mdogo, ambaye ndiye pekee aliyenusurika katika tukio hilo, Kijana huyo alifanikiwa kutoroka akiwa na Majeraha ya risasi kwenye mguu na mkono, huku wahasiriwa sita waliouawa; Kezzie Childs 42, Raymond Childs 42, Elijah Childs 18,Rita Childs 13, Kiara Hawkins 19 na Mtoto wa Kiaa ambaye hajazaliwa, aliyetambuliwa na Mamlaka kama “Baby Boy Hawkins”,