Bibi harusi afariki Ukumbini akimuimbia Mumewe

Sherehe ya harusi iliyofanyika siku ya Jumamosi Oktoba 26 Nchini Cameroon imegeuka kuwa vilio na huzuni baada ya Bibi harusi anayejulikana kama Sorelle Manuella kuanguka akiwa anaimba na kucheza wimbo maalum kwa ajili ya Mumewe.

Bi Harusi huyo aliyefariki kutokana na mshtuko wa moyo kwa mujibu wa ripoti za madaktari hapo awali watu wengi walidhani kuanguka kwake ilikuwa ni sehemu ya onyesholake kabla ya watukugundua na juhudi za kumpa huduma ya kwanza zikagonga mwamba.

Muda mfupi baada ya kupelekwa Hospitali madaktari walitangaza na kuthibitisha kuwa mwanamama huyo tayari amefariki.

Sorelle ameacha mume ambaye alifunga naye ndoa muda mfupi kabla ya kifo chake na binti watatu wachanga, mdogo zaidi akiwa na umri wa mwaka mmoja.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii