Mtahiniwa wa KCSE Azimia na Kukata Roho Akijiandaa Kufanya Mtihani Wake wa Mwisho

Hali ya sintofahamu imetanda Friends School Womulalu katika Kaunti ya Vihiga baada ya mtahiniwa wa KCSE, aliyetambulika kama Snider Undisa, kuaga dunia kabla ya kukamilisha mtihani wake wa mwisho. 

Mwalimu wake, Judy Ronoh, alitumia mitandao ya kijamii kushiriki huzuni yake na kutoa heshima kwa mwanafunzi aliyemlea kwa miaka minne. Mwalimu huyo aliyejaa huzuni alitoa rambirambi zake, akimkumbuka marehemu kama mtoto mzuri, mwenye nidhamu na daima mchangamfu. 

Judy alifichua kuwa huenda Snider alikuwa na kifafa, lakini alipenda shule na alihudhuria masomo licha ya changamoto za kiafya. 

Alielezea jinsi wiki hiyo imekuwa ngumu shuleni tangu msichana huyo alipofariki, akionyesha tumaini lake kwamba Mungu angemruhusu amalize mtihani wake wa mwisho na kupata matokeo yake.

Snider alizimia Jumapili kabla ya kifo chake na aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa uti wa mgongo baada ya kushindwa kupata fahamu kwa siku tatu.

Licha ya jitihada za kitabibu, alifariki Alhamisi jioni katika Hospitali ya Misheni ya Itando.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii