Iran imetangaza hivi punse siku ya Jumapili Novelba 24, 2024 kwamba majadiliano juu ya mpango wake wa nyuklia yatafanyika katika siku zijazo na Ufaransa, Ujerumani na Uingereza, nchi tatu ambazo ziliwasilisha nakala ya kulaani ukosefu wa ushirikiano wa Tehran katika suala hili.
Paris, Berlin na London, ikijumuishwa na Washington, zimeandika taarifa inayokosoa mpango wa nyuklia wa Tehran iliyowasilishwa wakati wa mkutano huko Vienna kwenye makao makuu ya Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (IAEA).
Nakala hiyo iliidhinishwa siku ya Alhamisi na nchi 19 kati ya 35 wanachama wa Bodi ya Magavana ya IAEA, na kuchochea hasira ya Iran ambayo ilitangaza kulipiza kisasi kuanzishwa kwa "utaratibu mpya" kwa mpango wake wa nyuklia.
Msemaji wa diplomasia ya Iran, Esmaïl Baghaï, amebainisha kuwa mkutano huo utafanyika siku ya Ijumaa, bila hata hivyo kubaini mahali utakapofanyika.
Uingereza ilithibitisha siku ya Jumapili kwamba mazungumzo haya yatafanyika. "Tunaendelea kujitolea kuchukua hatua zote za kidiplomasia kuzuia Iran kutengeneza silaha za nyuklia, ikiwa ni pamoja na hatua za kulipiza kisasi ikiwa ni lazima," Ofisi ya Mambo ya Nje ya Uingereza ilisema.
Mbali na faili hili, Iran itajadili na nchi hizi hali ya kikanda na kimataifa, "ikiwa ni pamoja na maswali ya Palestina na Lebanoni", Bw. Baghaï amesema katika taarifa yake kwa vyombo vya habari.
Iran inayounga mkono Hezbollah nchini Lebanoni na Hamas huko Gaza, makundi mawili ya Kiislamu yanayoopigana na Israel, adui mkubwa wa Tehran tangu kuja kwa Jamhuri ya Kiislamu mwaka 1979.
Tehran inatetea haki ya nishati ya nyuklia kwa madhumuni ya kiraia, haswa kwa nishati, lakini inakanusha kutaka kupata bomu la atomiki, hali ambayo nchi za Magharibi zinashuku.