Yanga Kumsajili Mshambuliaji Huyu Kutoka Uganda...Noma na Nusu
YANGA imeanza mikakati ya kuimarisha safu yake ya ushambuliaji katika dirisha dogo la usajili litakalofunguliwa Desemba 15 mwaka huu ambapo jina la mshambuliaji Bayo Aziz Fahad ndio kipaumbele chao cha kwanza.
Bayo mwenye umri wa miaka 26, inaripotiwa kuwa ameshafanya mazungmzo na kumalizana na vigogo wa Yanga ambapo wamefikia pazuri huku kilichobaki kwa mchezaji huyo ni kusubiri dirisha dogo ili ajiunge nayo.
Uwezo wa kufunga na kupiga pasi za mwisho ambao Bayo amekuwa nao unaonekana kuiridhisha Yanga ambayo ujio wa mshambuliaji huyo utasaidia safu yake ya ushambuliaji lakini pia kuwaongezea ushindani chanya washambuliaji waliopo kikosini ambao wanaonekana bado wanajitafuta.
Kwa sasa, Bayo ni mchezaji huru baada ya kuachana na MFK Vyskov inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Czech ambayo aliichezea mechi 42 na kuifungia mabao manane.
Kabla ya kujiunga na Vyskov, Bayo aliitumikia Ashdod inayoshiriki Ligi Kuu ya Israel ambako katika mechi 41 alizoichezea, alifunga mabao manane huku akipiga pasi moja ya mwisho.
Katika timu ya taifa ya Uganda, mshambuliaji huyo amecheza mechi 21 na kuhusika na mabao tisa, akifunga mabao manane (8)
Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii