Hata hivyo, wanachama wa magenge waliendelea na mashambulizi katika baadhi ya wilaya za mji huo wenye ghasia, baada ya mmoja wa viongozi wao kutoa wito Jumatatu jioni kwa serikali ya mpito kuachia ngazi.
Mpiga picha wa shirika la habari la AFP ameona watu wakichoma miili ya watu wanaodaiwa kuwa ni wa magenge barabarani, huku tairi zikiwa zimerundikana juu yao na kuichoma.
Maafisa walisimamisha lori lililokuwa limebeba wanachama wa genge katika kitongoji cha matajiri cha Petion Ville, saa 2:00 asubuhi Jumanne, msemaji wa Polisi ya Haiti, Lionel Lazarre, ameiambia AFP.