Kiambu: Mtoto Apatikana Hai Huku Polisi Wakigundua Miili ya Wazazi Wa Mtoto Huyo Yakutwa Imeoza

Polisi katika kaunti ya Kiambu wanachunguza kisa ambapo mtoto mchanga aligunduliwa akiwa amelala kando ya mwili wa mama yake uliooza mnamo Jumapili, Novemba 17. 

Baba yake mtoto huyo pia alipatikana amefariki katika nyumba hiyo hiyo, na kuzua maswali kuhusu hali iliyosababisha vifo vyao. 

Polisi walimpata mtoto huyo mchanga mwenye umri wa miezi 18, akiwa hai na kumpeleka hospitalini kwa matibabu. Uchunguzi wa polisi ulibaini kuwa mwanamume huyo aliripotiwa kumuua mkewe kabla ya kukutana na kifo chake mwenyewe. 

Marehemu alitambulika kwa jina la Rueben Ndede kutokana na Kitambulisho chake kilichopatukana mfukoni na polisi. Utambulisho wa mke haujathibitishwa.

Miili hiyo ilisafirishwa hadi katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City kwa ajili ya kuhifadhiwa huku uchunguzi kuhusu vifo vyao ukiendelea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii