Shambaboi wa Miaka 21 Atiwa Nguvuni na DCI Kufuatia Mauaji ya Ajuza wa Miaka 78

Polisi wanamzuilia kijana mmoja anayeshukiwa kuhusika katika mauaji ya ajuza wa miaka 78.

 Catherine Waceke alitoweka Jumamosi, Novemba 10, siku moja kabla ya mwili wake kugunduliwa ndani ya tanki la maji taka nyumbani kwake Nyathaini, Kasarani. Katika uchunguzi wao wa awali, wapelelezi walibaini kuwa mauaji hayo yalifanyika ndani ya boma la marehemu.

Mara moja msako ulianzishwa kwa Victor Ambeyi mwenye umri wa miaka 21, ambaye alimfanyia kazi marehemu. Msako huo ulifanikiwa kuwaongoza maafisa wa upelelezi hadi Kinoo, kaunti ya Kiambu, ambapo walimpata mshukiwa. "Mshukiwa, Victor Ambeyi, alipatikana katika maficho yake eneo la Valley la Kinoo katika Kaunti ya Kiambu ambapo mshukiwa alikuwa amefichwa na binamu yake, Collins Seda Wanjau, 22. Wawili hao walikamatwa," DCI alisema. 



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii