Aliyekuwa Katibu wa chama cha mapinduzi wilayani Kilolo Mkoani Iringa Christina Kibiki amevamiwa na watu wasiojulikana na kuuwawa nyumbani kwake kwakupigwa risasi kifuani.
Tukio hilo lakuvamiwa na kuuwawa limetokea usiku wakuamkia leo katika kitongoji cha Banawanu kata ya mseke nje kidogo ya mji wa Iringa
Katika hatua nyingine Chama cha Mapinduzi, kimetoa taarifa kuhusu tukio hilo ambapo taarifa yake imeeleza kuwa chama kimepokea kwa mstuko mkubwa taarifa hizo
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Novemba 13, 2024 na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenezi na Mafunzo, Amos Makalla imesema kuwa marehemu alikuwa anajindaa kuhudhuria semina elekezi kwa Makatibu Mjini Dodoma kesho.
"Tunawaomba wanachama wetu wawe watulivu wakati vyombo vya dola vikifuatilia na kuchunguza tukio hili, ili wahusika waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheriaā€¯ alisema.