Mwanamke mmoja kutoka Mji Mema, Songea, Tanzania, amejawa na huzuni baada ya mtoto wake kupotea akiwa kwenye sehemu yake eneo la kazi.
Gabriella alikuwa akifanya kazi kwenye saluni yake Jumatatu, Novemba 4, wakati mtoto wake alipoibiwa.
Mama huyo wa watoto wawili alieleza matukio yaliyosababisha binti yake, Glory James, kuchukuliwa na mwanamke asiyejulikana. Gabriella alikuwa akimtengeneza mteja wake nywele asubuhi wakati mshukiwa alipokuja na kuwasalimia. “Walionekana kufahamiana, walikuwa wakiwasiliana kupitia simu zao wakitumana meseji, akauliza bei za huduma fulani nikamweleza, akasema mdogo wake aliyekuwa nyumbani alitaka kusongwa."
"Baadaye alibaini kuwa mtoto wangu wa miezi 11 alikuwa amejichafua Aliniuliza nimbadilishe nepi na nguo, jambo ambalo nilifanya," Gabriella alishiriki. Gabriella alipiga ripoti kwa polisi kufuatia kutoweka kwa mwanawe.
Gabriella alisema mwanamke huyo wa ajabu alimnyanyua Gladys na akajaribu kumtuliza huku mamake akimalizia kunyoa nywele za mteja wake. "Niliwaza angerudi kwani alikuwa ameenda kutafuta mafuta ya nywele ambayo nilikuwa nimemwambia sina.
Nilisubiri hadi saa tisa mchana, na hapo ndipo nilipotambua kwamba binti yangu alikuwa amechukuliwa. Sikuweza kukumbuka sura za wale wanawake, lakini niliarifu polisi," alisema mwanamke huyo aliyekuwa na huzuni.