Wakalini watakiwa kuungana kulinda uchumi wa nchi

Vyama vya Mawakili nchini vimetakiwa kushirikiana kwa pamoja kusaidia wananchi katika kupata haki lakini pia kupunguza changamoto za uhujumu wa uchumi kwa wawekezaji wanaotaka kuwekeza ndani na nje ya nchi.

Wito huo umetolewa na Wakili Mkuu, Dkt. Ally Possi mara baada ya kikao chake na viongozi wa Mawakili nchini ambapo wameandaa mpango utakaosaidia kuongeza weledi, kulinda uchumi pamoja na kulinda rasilimali nchini.

"Shughuli ambazo tunazifanya nyingi zikiwa ni za Kimahakama, nyingi ni za kuwasaidia wananchi ambao ni wateja wetu nyingi, kwa lugha nyepesi zote zikiwa ni za kisheria ambazo wote tunafanya tumeona kuna haja ya kushirikiana na kuangalia mawanda ambayo sisi kama wanasheria wa Tanzania tunaweza tukashirikiana, kwahiyo Public barner na TLS, tayari wameshaandaa memorandum ambayo itapitia taratibu zxa kiserikali na itakapokamilika tutasainishana" , alisema Dkt.Ally Possi-Wakili Mkuu.

Kwa upande wake Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali, Amedeus Shayo, anasema ushirikiano huo ni utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa 2022 kuonesha nguvu yetu katika kulinda uchumi wa nchi.

"Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Daktari Samia Suluhu Hassan, wakati akizindua chama chetu, tarehe 22, alitoa agizo aliagiza kuwa nyie Mawakili ni Jeshi la kalamu na karatasi tumieni hizo nyezo kulinda uchumi wetu, kwahiyo tumekutana hapa kuangalia ni jinsi gani tunaweza kulinda uchumi wetu" , alisema  Amedeus Shayo-Rais wa Chama cha Mawakili wa Serikali.

Nae Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika TLS anaelezea namna ambavyo watatekeleza mashirikiano hayo.

"Katika kushirikishana uzoefu, kujengeana uzoefu na katika kutekeleza majukumu yetu kwa namna ambayo  kuwa na tija kwa Taifa na itkuwa na tija kwa Taifa kiuchumi, kijamii na siasa zinazoendelea katika taifa letu, kwahiyo moja ya mambo tuliyozungumzia ni kusaini makubaliano, kati ya Tanganyika law society na wenzetu wa public bar na kwa namna ya kuhusiana namna ya kufanya shughuli zetu namna ya kujengeana uwezo na namna ya kushirikishana uzoefu katika maswala mbalimbali", alisema  Boniface Mwabukusi-Rais wa TLS.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii