Ukraine inaishtumu Russia kushambulia meli ya nafaka

Ukraine Alhamisi iliishtumu Russia kwa kutumia makombora ya kimkakati kushambulia meli ya nafaka ya kiraia katika shambulizi la kombora katika bahari ya Black Sea karibu na Romania, nchi mwanachama wa NATO, na kuzidisha mvutano kati ya Moscow na muungano huo wa ushirika wa kijeshi.

Rais Volodymyr Zelenskiy alisema meli hiyo iliyokuwa inasafirisha nafaka kuelekea Misri ilishambuliwa usiku wa Jumatano na kombora la Russia mara tu baada ya kuondoka kwenye eneo la bahari ya Ukraine.

Alisema hakuna vifo vilivyotokea.

Balozi wa Marekani nchini Ukraine “alilaani vikali” shambulizi hilo na kusema Russia ilihusika. Msemaji wa Umoja wa Mataifa alisema tukio hilo ni “ukumbusho mkubwa” wa vitisho ambavyo meli za kiraia bado zinakabiliana navyo katika bahari ya Black Sea.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii