Mahakama ya Iran yampa adhabu ya kifo mwanajeshi

Mahakama ya Juu ya Iran, imekubali hukumu ya kifo iliyotolewa kwa mwanachama wa tawi la kujitolea la Jeshi la Mapinduzi la nchi hiyo ambaye alivamia nyumba wakati wa maandamano ya 2022 ya kupinga kifo cha Mahsa Amini na kumuua mzee wa miaka 60, wakili wake amesema Jumanne.

Hukumu iliyotolewa kwa mwanachama wa Basij inaashiria wakati adimu kwa Iran kuviwajibisha vikosi vyake vya usalama, ambavyo viliendesha umwagaji damu, kwa miezi kadhaa dhidi ya wapinzani wote kuhusu kifo cha Amini.

Zaidi ya watu 500 waliuawa na zaidi ya 22,000 waliwekwa kizuizini. Tangu wakati huo, Iran imewaua waandamanaji wengi waliokuwa wakishikiliwa baada ya msako na kushutumiwa kuuwa vikosi vya usalama, baada ya kesi za siri kukosolewa na wanaharakati nje ya nchi.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii