Wa South Africa Hawamtaki Chriss Brown Afanye Show Nchini Kwao

Kikundi cha Utetezi wa Wanawake (Woman Change) Afrika Kusini kimeanzisha Kampeni ya kutaka kusitishwa kwa Tamasha lijalo la Msanii #ChrisBrown Nchini humo Disemba 14.2024 kwa madai ya kuwa anahistoria mbaya ya unyanyasaji wa kijinsia huku wakitaja hukumu yake kutokana na kumshambulia aliekuwa mpenzi wake 2009 #Rihanna

.

Tamasha hilo linaenda sambamba na Siku 16 za Kupinga Unyanyasaji wa Kijinsia nchini Afrika Kusini

.

Ombi la kupiga marufuku show ya #Brown limekusanya zaidi ya sahihi 20,000, huku mawakili wakiitaka Idara ya Masuala ya Ndani ya Nchi kumfutilia mbali viza yake.

.

Wakati mashabiki wengi, wakiwemo wanawake, wakiisubiri kwa hamu show ya #CB, wanaharakati wanasisitiza kuwa kumruhusu kutumbuiza kunadhoofisha mapambano dhidi ya ukatili dhidi ya wanawake.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii