Mwanamitindo na mfanyabiashara maarufu, Zari Hassan, ametangaza rasmi kuachana na mume wake, Shakib Cham, baada ya kuwa pamoja kwa takribani miaka mitano.
Zari amethibitisha taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa Instagram, ambapo amesema yeye na Shakib wamefikia uamuzi wa kutengana baada ya kushindwa kutatua tofauti zilizokuwepo katika mahusiano yao licha ya juhudi mbalimbali za kuyarekebisha.
Katika ujumbe wake, Zari amesema uamuzi huo haukuwa rahisi kuufikia, lakini baada ya kutafakari kwa kina kuhusu mustakabali wao, wameona ni hatua sahihi kwa pande zote mbili.