Familia ya mwenyekiti wa kwanza wa Halmashauri ya Mji wa Siaya, Mzee John Oruenjo Umidha, imefichua kuwa atazikwa ndani ya nyumba yake.
mwanae Koruenjo, wamechimba kaburi kwa ajili ya kujiandaa kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika Jumamosi, Septemba 28.
Tamanio lake la mwisho ilikuwa azikwe ndani ya nyumba yake, na hicho ndicho kinachofanyika sasa,” alisema manae.
Wazee wa jamii ya Waluo huko Siaya walithibitisha kuwa desturi ya mazishi ni ya kawaida na inakubalika kitamaduni, wakibainisha kuwa ni muhimu kuheshimu matakwa ya mwisho ya marehemu na “Tunafanya jambo ambalo halijafanyika kwa muda mrefu.
Mzee mwingine alisema kuwa kwenda shule hakuwezi kumfanya mtu kusahau kuhusu mila za kitamaduni.
“Najua baadhi yenu mnasema kwamba ukienda shule unapaswa kusahau utamaduni. Hii si kweli kabisa; jambo moja tunalopaswa kujua ni kwamba tunapaswa kujua mizizi yetu, ambayo inatufanya tuishi maisha yenye nidhamu,” alisema.