Wafanyabiashara stendi ya Moshi wafunga maduka yao

Maduka yote ya Stendi Kuu ya Moshi mkoani Kilimanjaro yamefungwa leo kutokana na mgomo wa wafanyabiashara hao ambao wanadai Kodi inayotozwa stendi hapo ni kubwa isiyo rafiki.


Hadi Sasa wafanyabiashara hao wamekusanyika nje ya maduka yao ili kuondoka na maazimio ya nini kifanyike. 


Hayo yanajiri kukiwa na taarifa za ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kuzuru mkoa wa Kilimanjaro mnamo mwezi Agosti mwaka huu.


Awali katika ziara ya Katibu wa zamani wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama cha Mapinduzi Paul Makonda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi hiyo wafanyabiashara walifikisha kero ya kodi wanazolipa stendi hapo ni kubwa zinawaumiza wao na wananchi kwa ujumla.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii