Venezuela: Rais Nicolas Maduro achaguliwa tena kwa muhula wa tatu, upinzani walalamikia udanganyifu

Rais wa Venezuela Nicolas Maduro ameshinda uchaguzi wa urais Jumapili, Julai 28, kwa asilimia 51.20 ya kura - sawa na kura milioni 5.15 -, tume ya uchaguzi imetangaza Jumatatu, Julai 29, ingawa kura kadhaa kutoka sanduku la kura zinaonyesha ushindi wa upinzani. Kwa hivyo alishinda muhula wa tatu wa miaka sita kama mkuu wa nchi, baada ya kampeni kali iliyogubikwa na tuhuma za upinzani kuhusu vitisho na hofu ya udanganyifu mkubwa.

Viongozi wa upinzani waliokuwa mbele katika uchaguzi huo, walitangaza Jumapili jioni kwamba walikuwa na "sababu za kusherehekea ushindi wao", huku wakiwataka wafuasi wao kufuatilia vituo vya kupigia kura ili kuhakikisha shughuli za kuhesabu kura zinaendelea vizuri. "Tunaomba Wavenezuela wote wawepo kutazama jinsi zoezi la uhesabiji kura linavyoendelea. Tumepambana miaka yote kwa siku hii, hizi ni dakika muhimu,” alisema kiongozi wa upinzani, Maria Corina Machado, aliyetangaza kuwa hastahili na nafasi yake kuchukuliwa na Edmundo Gonzalez Urrutia kwa muda mfupi.



Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii