Washukiwa 2 Walionaswa kwenye CCTV Wakiibia Wagonjwa Watiwa Mbaroni

Washukiwa wawili walitiwa mbaroni kwa madai ya kuiba wagonjwa wasiofahamu katika hospitali ya Machakos Level 5.


Washukiwa hao wawili walikamatwa baada ya mmoja wao, Peter Mutavi, kunaswa kwenye picha za CCTV akimuiba mgonjwa katika idara ya radiolojia ya kituo hicho.

Mgonjwa mmoja aliteta hospitalini baada ya simu yake kupotea, hali iliyowafanya maafisa wa usalama kukagua kanda za CCTV zilizofichua kuwa Mutavi ndiye mshukiwa. 

"Nilishuku simu yangu iliibiwa na mwanamume niliyekutana naye eneo la X-ray.

Ndiposa uchunguzi ulipoanza, wakanionyesha mshukiwa. Pia tuliona mwanamke mwingine kwenye picha za CCTV akiibiwa," mwathiriwa wa kike alisema.

Mshukiwa aliwaambia polisi kuhusu jamaa mwingine kwa jina Francis Mumo, ambaye alidai kuwa ni mshirika wake katika wizi wa hospitali. Baada ya uchunguzi zaidi, polisi walimpata Mumo akiwa na simu inayoshukiwa kuibiwa kutoka kwa mgonjwa.

Afisa Mkuu wa Kitengo cha Afya Machakos Simon Mwako, alisema kuwa malipo yote katika hospitali hiyo huchakatwa kupitia simu, hivyo kuwarahisishia wahalifu kuwalenga wagonjwa.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii