Musa Mbaroni Kwa Kumuua na Kumkata Vipande Vipande Ezenia

Jeshi la Polisi linamshikilia Abdallah Miraji maarufu kama Musa (42)mkazi wa Dar es Salaam kwa Kosa la kumuua kwa kumkata kata mpenzi wake Ezenia Stanley Kamana (36) na kisha kutupa viungo vya mwili wake maeneo mbalimbali.


Bi.Ezenia aliripotiwa kutoweka mnamo tarehe 19 Agosti, 2024 Jeshi la Polisi lilianza uchunguzi na kubaini kwamba alikuwa na rafiki yake wa kiume Bw.Abdallah na ndipo akakamatwa.


Awali Mtuhumiwa amekana kumfahamu Bi.Ezenia, baada ya Viroba Vinne vyenye viungo vya mwili vikiwemo paja, vipande vya mikono, utumbo na nguo maeneo ya kunduchi,ndipo Mtuhumiwa alikiri kufanya uhalifu huo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii