Israel yadaiwa kuuwa raia wa Palestina 28

Mashambulizi ya Israel, yamewauwa raia 28 wa Palestina katika mapigano mapya ya Gaza, ikijumuisha mwanamke na watoto wake sita kwa mujibu wa maafisa wa afya wa Palestina.

Mashambulizi yamefanyika kabla ya ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Antony Blinken, katika hatua mpya ya kufikia makubaliano ya kusimamisha mapigano na kuzuiwa vita vya miezi 10 vya Israel na Hamas.

Mazungumzo yanayo chukuwa muda mrefu ya kusimamisha mapigano yameshafikisha miezi kadhaa sasa.

Maafisa kwa nyakati tofauti wamesema kwamba mazungumzo yalifikia muafaka, lakini kamwe hayajawahi kumalizika.

Marekani na wapatanishi wengine Misri na Qatar amesema wamekaribia kufikia muafaka baada ya mazungumzo ya siku mbili mjini Doha wiki iliyopita, lakini Hamas walionyesha kupinga kutokana nay ale yaliyokuwa matakwa mapya ya Israel.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuanza tena mjini Cairo katika siku kadhaa zijazo.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii