Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ndege ya kijeshi isiyo na rubani inayoshukiwa kutoka nchi jirani ya Uganda ilianguka katika jimbo la Ituri. Jeshi la Kongo limetangaza kufunguliwa kwa uchunguzi, huku Uganda ikishushiwa lawama na Umoja wa Mataifa kuwa inawasaidia waasi wa M23.
Habari hizo zilithibitishwa siku ya Jumanne na mamlaka ya kijeshi ya jimbo la Ituri. Hakika, usiku wa Jumatatu iliyopita, ndege ya kijeshi isiyo na rubani yenye rangi ya Uganda ilianguka katika kijiji cha Katoni, katika eneo la Ezekere groupement, huko Djugu. Katika picha zilizorushwa na jeshi na wakazi, bendera ya Uganda inaonekana kwenye ndege hiyo.
Luteni Jules Ngongo, msemaji wa jeshi huko Ituri, alitangaza kufunguliwa kwa uchunguzi: "Kuna ndege isiyo na rubani ya kijeshi ambayo ilianguka katika ardhi ya Kongo. Ndege hiyo inawezekana ilitokea Uganda kwa sasa, tumeokoa mabaki ya chombo hiki cha kijeshi. Kwa sasa tunatatmii ili kujua zaidi. Je! ilikuwa ni ndege isiyo na rubani? Na kwa nini ndege hii isiyo na rubani ilikiuka anga ya Kongo huko Ituri? Tunaamini kuna haja ya uchunguzi zaidi. "
Mnamo tarehe 7 Agosti, Luteni Jenerali Lubaya Nkashama, gavana wa Ituri, alitahadharisha vyombo vya usalama kwa njia ya simu kuhusu uwezekano wa wapiganaji kupenya na kuingia katika mkoa wa Ituri kutoka Uganda kupitia kijiji cha Kariabugongo. Kwa mujibu wa wakaazi na viongozi waliohojiwa na waandishinwa habari, jeshi la Kongo limeimarisha wanajeshi wake katika eneo hilo ili kuzuia mashambulizi yoyote yanayoweza kutokea.