Mbuzi wazikwa makaburini na sanda

Mbuzi wawili jike na dume wamekutwa wamekufa na kufukiwa makaburini wakiwa wamevalishwa sanda mithili ya mwili wa mtu aliyekufa kisha kufanyiwa maandalizi ya maziko makaburini.


Tukio hili limetokea katika Kijiji cha Mwailanje Kata ya Kimaha Wilayani Chemba Mkoani Dodoma kisha kusababisha taharuki kwa wananchi wa kijiji hicho.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hili wameeleza kuwa hayo ni matendo ya kishirikina yanayoendelea kukithiri kijijini hapo na kuleta taharuki kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Mwailanje  Bakari Mkamba amethibitisha tukio hilo na amewataka wananchi wenye tabia hizo kuacha mara moja kwani linaleta taharuki kwa wananchi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii