Karibu makombora thelathini ya Hezbollah yarushwa kuelekea Israeli

Iran ilionya. Hezbollah inaonekana imeanza jibu lake lililotangazwa, baada ya karibu makombora thelathini kurushwa kuelekea Israeli usiku wa Jumamosi Agosti 3kuamkia Jumapili Agosti 4. Hii inafuatia mashambulizi kadhaa ya Israel kusini mwa Lebanon, likiwemo lile lililomuua Fouad Chokr, kiongozi wa kijeshi wa Hezbollah, siku ya Jumanne Julai 30. 

Hezbollah pia kinataka kuonyesha mshikamano na Wapalestina na kinataka kulipiza kisasi kifo cha kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Hamas, Ismaïl Haniyeh, aliyeuawa pia katika shambulio linalohusishwa Israel siku ya Jumatano Julai 31.

"Hezbollah imeongeza eneo jipya la Beit Hillel (kaskazini) linalokaliwa walowezi kwenye orodha ya maeneo yanayotakiwa kulengwa na imelishambulia kwa mara ya kwanza kwa makumi ya maroketi," kundi hili linalounga mkono Iran limesema katika taarifa yake. Jeshi la Israel kwa upande wake limehakikisha kwamba "marombora 30 yalitambuliwa yakirushwa kutoka Lebanon" wakati usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, "mengi yao yakiwa yamenaswa".

Mvutano katika kilele chake katika kanda

"Hakuna majeraha yaliyoripotiwa," kulingana na vikosi vya jeshi la Israeli, ambavyo vimebainisha kuwa "wamepiga" eneo la Hezbollah ambapo makombora yalirushwa kusini mwa Lebanon. Tel Aviv na Haifa "ni miongoni mwa maeneo yatakayolengwa," limesema Gazeti la kila siku la Iran Kayhan. Wahouthi pia walitishia Israeli kwa "jibu la kijeshi".

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii