Mamlaka nchini Iran imetangaza kipindi cha siku tano kwa watu wanaotaka kuwania katika uchaguzi wa urais wa tarehe 28 ya mwezi Juni mwaka huu kuwasilisha maombi yao.
Uchaguzi huo unatarajiwa kufanyika baada ya aliyekuwa rais wa taifa hilo Ebrahim Raisi kufariki katika ajali ya helikopta mapema mwezi huu akiwa na maofisa wengine saba wa serikali.
Uchaguzi huo umepangwa kufanyika wakati huu ambapo raia wa Iran bado wanagali na maswali kutokana na ajali hiyo ya tarehe 19 ya mwezi Mei.
Zoezi hizo limeratibiwa kufanyika wakati huu pia kukiwa na hali ya wasiwasi kati ya Tehran na Marekani pamoja na maandamano ya mwaka wa 2022 yaliochochewa na kifo cha Mahsa Amini akiwa kizuizini.
Licha ya kuwa kiongozi wa juu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei, 85, ndiye mwenye kutoa maamuzi ya mwisho kuhusiana na masuala ya kitaifa, marais wa awali walionekana waliielekeza Iran kwenye mizozo na kuongezeka kwa uadui na nchi za Magharibi.
Katika kipindi cha siku tano wagombea kati ya umri wa miaka 40 hadi 75 na wenye shahada ya uzamivu ndio wanaotarajiwa kuwasilisha maombi yao.