Mahakama ya wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya imemuhukumu kwenda jela miaka miwili au faini ya milioni 5 Shadrack Chaula kijana ambaye video yake ilisambaa mitandaoni akimkashifu na kuchoma picha inayomuonesha Rais Samia Suluhu Hassan.
Ikumbukwe kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya SACP Benjamin Kuzaga,Julai 2 mwaka huu ilieleza kuwa mnamo Juni 30, 2024, mtuhumiwa huyo ambaye ni msanii wa sanaa ya uchoraji alijirekodi video fupi akitamka maneno makali ya kumkashifu Rais Samia huku akichoma picha inayomuonesha Rais na kuisambaza mitandaoni.