Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza
linawashikilia watu wanne ambao:- 1.Robert Daud, miaka 42, mume wa
mganga, mkazi wa katunguru, 2. Sylivester Renetus, Miaka 30, Mkazi wa
katunguru, 3. Ryabakamba Sekelwa, Miaka 30, mwanamke, mganga wa
kienyeji, mkazi wa katunguru na 4. Elizabeth Jackson, miaka 23, wote
wakazi wa Katunguru Senegerema, kwa tuhuma za Mauaji ya Respikius
Anastaz, Miaka 55, Dereva tax aliyekua anapaki maeneo ya Dampo-mwanza,
Mkazi wa Isamilo Mwanza, aliyeuawa ndani ya gari aina ya IST rangi
nyeusi yenye namba T.143 DHV, kwa kukabwa na kamba, kuchomwa visu
shingoni na kutobolewa macho hadi kufa, kitendo ambacho ni kosa la
jinai.
Tukio hilo limetokea 26.01.2022 majira ya 22:15hrs usiku
katika kijiji cha Kasungamile, Wilayani Sengerema, hii ni baada ya
Dereva tax ambaye ni Marehemu kwa sasa kukodiwa na mtuhumiwa Sylivester
Renatus akiwa na mkewe Elizabeth Jackson toka Buzuruga Mwanza kwenda
Sengerema na walipofika maeneo ya Kijiji cha Kasungamile walitekeleza
unyama huo. Inadiwa kuwa baada ya kufanya mauaji hayo walikwenda kwa
mganga wa kienyeji ili wasafishwe aitwaye Ryabakamba Sekelwa ambaye
amekamatwa pamoja na mumewe.
Polisi wakiwa doria majira 22:00hrs
walikuta gari hiyo ikiwe imetelekezwa katikati ya barabara ndipo
ufuatiliaji wa haraka ulifanyika na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa
pamoja na mganga wa kienyeji. Kiini cha tukio hilo ni kuwania mali
(kupora gari). Tayari gari imepatikana ikiwa imefungwa namba bandia
mbele na nyuma ambayo ni T 620 CGN na eno la tukio kumepatikana Visu
viwili, panga moja, nyundo moja na simu mbili aina ya TECNO moja kubwa
na nyingine ndogo na kamba moja.
Ndugu wanahabari, tarehe
29.01.2022 majira ya 19:30hrs, huko mtaa wa Ng’washi, kata ya Buhongwa,
Wilaya ya Nyamagana, Nicholus Telesphory, miaka 25, Mkazi wa Malimbe,
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mt.Augustine –Mwanza, aliuawa na kundi la
wahalifu kwa kupigwa mawe na fimbo sehemu mbalimbali za mwili wake kwa
tuhuma za wizi wa Televisheni na baadae kufariki dunia wakati akipatiwa
matibabu katika hospital ya Mkoa Sekou Toure .
Baada ya
upelelezi wa kina Jeshi la Polisi limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa
watano kuhusiana na tukio hilo ambao ni 1. Thobias Lucus @ Joseph, miaka
25, mkazi wa Nyanembe, 2.Alex Madoshi @ Junior, miaka 20, Mkazi wa
Ng’washi, 3.Yusuph Mwandesha, miaka 25, mkazi wa Ng’washi, 4. Samwel
Masalu @ George, Miaka 25, mkazi WA Lwanhima Na 5.Nyanda Madirisha,
miaka 19, Mkazi WA Ng’washi, wote ni waendesha bajaji. Chanzo cha tukio
hilo ni kujichukulia sheria mkononi. Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza
linakamisha upelelezi wa mashauri haya na baadae watuhumiwa wote
watafikishwa mahakamani ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa
dhidi yao.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linatoa onyo kwa
baadhi ya wananchi wenye tabia ya kujichukulia sheria mkononi na kuwania
mali kuacha mara moja kwani ni kosa kisheria na endapo watabainika
watashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. Sambamba na hilo linawasisitiza
wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi ili liweze
kudhibiti vitendo vya kihalifu na wahalifu katika Mkoa wetu.