Mahujaji wakusanyika Saudia kuanza ibada ya Hijja

Mamia kwa maelfu ya mahujaji wa kiislamu wanaanza leo ibada Hijja katika mji mtakatifu wa Makkah nchini Saudi Arabia kutimiza moja ya nguzo kuu za dini hiyo yenye zaidi ya waumini bilioni 2 kote ulimwenguni.


Hadi siku ya Jumanne zaidi ya waumini milioni 1.5 walikuwa wamewasili nchini Saudia kwa ibada hiyo.

Hivi leo ibada hiyo itaanza rasmi kwenye eneo la jangwa la Mina na kesho Jumamosi mahujaji watafanya safari ya siku nzima kuelekea kwenye mlima Arafat eneo inakoaminika Mtume Muhammad (S.A.W) alitoa hotuba ya mwisho kwa umma wa Waislamu kiasi miaka 1,400 iliyopita.

Ibada ya Hijja huitimishwa kwa sherehe za Eid Al-Adhaa zitakazofanyika siku ya Jumapili.

Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii