Mashambulizi ya Wahouthi yaazidi kusumbua usafirishaji bahari ya Sham

Mashambulizi yasiyosita dhidi ya meli za kimataifa yanayofanywa na wanamgambo wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran nchini Yemen yanaathiri juhudi za kibiashara na misaada licha ya majaribio ya Marekani na washirika wake kupunguza athari hizo.

Ripoti iliyotolewa karibuni ya shirika la ujasusi la ulinzi la Marekani (DIA) imegundua mashambulizi ya Wahouthi kwenye meli katika bahari ya sham na ghuba ya Aden yameathiri takriban makampuni 29 katika nchi zaidi ya 65, na kusababisha gharama kubwa katika nyanja nyingi.

“Kufikia katikati ya Februari, malipo ya bima ya usafiri katika bahari ya Sham yamepanda kwa kati ya asilimia 0.7 na 1 ya jumla ya thamani ya meli, ikilinganishwa na chini ya asilimia 0.1 kabla ya Desemba 2023,” kwa mujibu wa ripoti ya DIA.

Ripoti hiyo pia ilibainisha makampuni ambayo yanaendelea kuvuka eneo hilo yanakabiliwa na ongezeko la gharama za bima ya ziada kwa sababu ya hatari ya vita na nyongeza kwa wafanyakazi wa melini.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii