Hakuna abiria aliyeponea katika ajali ya ndege nchini Malawi: Rais Chakwera

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amethibitisha kuwa hakuna abiria aliyepona katika ajali ya ndege iliokuwa imembeba makamu wa rais Saulos Chilima na watu wengine tisa.


Makamu wa rais wa Malawi, Saulos Chilima,mwenye umri wa miaka 51 ni miongoni mwa abiria 10 waliouawa katika ajali ya ndege ndogo ya kijeshi kaskazini mwa taifa hilo.


Kwa mujibu wa taarifa ya rais Lazarus Chakwera kupitia televisheni ya kitaifa, ndege hiyo imepatikana baada ya zoezi la karibia siku moja kuitafuta na kwamba hakuna yeyote aliyeponea.


Mke wa rais wa zamani Bakili Muluzi, Shanil Dzimbiri ni miongoni mwa abiria waliokuwa kwenye ndege hiyo kwa mujibu wa taarifa ya rais Chakwera.


Taarifa zaidi zinasema abiria wengine saba na wafanyikazi watatu ambao ni wanajeshi walikuwa kwenye ndege hiyo.


Abiria hao walikuwa wanasafiri katika eneo la Mzuzu kwa ajili ya mazishi ya waziri wa zamani katika serrikali ya Malawi.


Pata Habari Kupitia Mitandao Yetu Ya Kijamii